Kama una nia au lengo
la kuanza kujitengenezea pesa kutoka youtube au google na una mbinu kidogo au
hujui kabisa mahali pakuanzia basi leo umepata kitu kitakachokusaidia kutimiza
lengo hilo. Kuna mambo machache sana ya kuzingatia ili kuweza kufanikisha jambo
hili ukiachana na ule utalamu au ujuzi wa kutumia mtandao kwa maana ya internet
fauatayo ni muhimu zaidi kuyafahamu:
Youtube ni bidhaa ya google. Amini kuwa unaweza kutengeneza pesa youtube
kwa sababu watu wengine pia wanafanya hivyo. Unaweza kutengeneza pesa kutoka google
bila hata kuitumia youtube. Google Adsense (Hii ndio hutoa kibali
cha wewe kupata pesa)
Google ni kampuni kubwa
ambayo ina huduma nyingi ikiwepo hii ya youtube na zingine nyingi zinazoweza
kukufanya utengeneze pesa endapo utaweza kuzifahamu na kuzitumia kwa lengo
hilo; hivyo youtube ukiitumia kama moja ya huduma za google unaweza kuingiz
pesa kubwa sana.
NAMNA
YA KUPATA PESA KUTOKA YOUTUBE
Ili uweze kupata pesa
kutoka youtube itakubidi kuyafahamu na kuyafanya haya yafuatayo ni marahisi
sana kama una nia na baada ya muda kidogo unaweza kuwa shuhuda wa watu wengine
au kuwaelekeza pia.
- · Fungua email ya google kwa maana ya www.gmail.com ili upate nafasi ya kuweza kujisajili Youtube
- Baaada ya kufungua email hio fungua youtube channel kwa kutumia email yako hio hapo juu na channel yako unaweza kuipa jina lolote unalotaka; kwa mfano, HELA TIME, MTONYO DAY nakadhalika.
- Anza kuweka vitu kwenye channel yako hio na kuwashirikisha watu wavione. Vitu hivi vinaweza kuwa video au audio (sauti) zinazoelezea au kusikika kuhusu kitu fulani
BAADA
YA HAPO HAYA YATAFATA
Baada ya kuendelea kutoa
vitu vyako na watu wakavipenda watajiunga na channel yako kwa maana ya kusubscribe
ili kila utakapoweka vitu wavione bila kuwambia na utakuwa unaona namba ya watu
au wafuatiliaji wako inaongezeka kwe nye sehemu ya subscribers. Ukisha fikisha
idadi ya wafuasi (subscribers) kuanzia elfu moja (1000) utaomba kuunganishwa na
kitu kinachoitwa Google Adsense ili
uanze kulipwa pesa kulingana na watu wanaotembelea na kuangalia vitu kwenye
channel yako. Lakini lazima hao
subscribers wapatikane ndani ya kipindi kisichozidi mwaka mmoja tangu
umefungua channel yako youtube, ukizidisha mwaka hujafanikiwa kuwapata hoa 1000
hutoweza kupata Adense na kwa maana hio hutoweza kupata pesa. Hii nayo utatumia
email yako ile uliyofungua kupitia www.gmail.com.
Baada ya kuomba
kuunganishwa na hii adsense na kupata ndani siku kadhaa utafanya settings kwa
maana ya mfumo wa nama ya kuonesha matangazo kwenye channel yako ili upate pesa
kwa sababu lengo kuu la kuomba adsense ni kuwaomba google wapitishe matangazo
yao kwenye channel yako ili watu wako wayaone na ulipwe pesa.
Baada ya kumaliza hilo
utaenda kwenye akaunti yako ya google adesense kuweka njia ya wewe kupokea
malipo kwa maana ya akaunti ya banki. Na hapo utabakia kuendelea kuweka vitu
kama kawaida watu wanavyopenda kuona au kusikiliza na kujipatia pesa.
KUTENGENEZA
PESA KUTOKA GOOGLE BILA HATA KUITUMIA YOUTUBE
Hii ni njia mabayo
unaweza kuachana na youtube kabisa ila bado utahitaji kitu muhimu sana kinaitwa
Google
Adsense kulifanikisha hili pia. Hapa ni kwa wale wanotumia blogs,
website na Apps za simu kufikisha vitu vyao kwa watu.
Haya ni ya muhimu sana
kuyafahamu ili kuweza kupata pesa kutoka google kupitia blogs na website.
·
Blogger na Blog
Kama niivyosema mwanzo
kuwa google wana huduma nyingi sana pia hizi ni zao; blogger na blog ambazo
husaidia mtu kufungua blog yake au website kwa kutumia email yake na kuanza
kuchapisha makala ambayo watu watayasoma na yeye akalipwa. Makala haya yanaweza
kuwa katika mtindo wa maandishi, sauti (audio), picha na video.
Kwa lugha yoyote ile duniani.
Hawa nao wanaotumia
njia hii wataomba kuunganishwa na google adsense ili walipwe pesa kama ilivyo
kwa youtube kwa sababu pia nao wataonesha matangazo ya google kwenye website na
blog zao.
Haya yote ni kwa
utaratibu unaotumiwa na google kwa kipindi hiki mwaka huu wa 2018 japo zamani
haikuwa hivi kwa maana ilikuwa rahisi zaidi hasa youtube.
Yapo mengi kuhusu jambo
hili ambalo mtu yeyote anaweza kulifanya na kujipatia pesa kutoka google na
huduma zao ila kwa sasa tunaishia hapa nadhani umepata mwanga kidogo au
umefahamu ulilokuwa hujui. Hivyo basi kama unadhani kuna swali au unahitaji
msaada basi:
wasilina nasi kwa simu namba 0743536577 au email: gericml@gmail.com
NAMNA YA KUTENGENEZA PESA KUTOKA GOOGLE NA SIMU YAKO
Reviewed by Geric Media Live
on
September 20, 2018
Rating:

No comments: