PESA ZIKO HAPA (SOUND CLOUD) (Part 2)


Karibu tena katika mwendelezo wa namna ya kutengeneza pesa kupitia online platform mbalimbali ususani soundcloud na audiomack. Kama ilivyo platform maarufu na yenye vikorokoro vingi (Youtube) na masharti magumu yanayo wazuia walio wengi kuweza kupata hela kutoka youtube. Na kama umepitwa na machapisho yaliyotangulia basi bofya hapa ili uweze kwenda hatua kwa hatua. 
Hapa leo tumekusogezea njia na mahitaji muhimu unayoweza kufanikisha hili. Kwanza kabisa taunze kuzifahamu hizi platform 2 yaani sound cloud na audio mack.
Hizi zote ni sehemu ambayo inaruhusu kupakia (upload) vitu vyoye katika mfumo wa audio yaani sauti kwa maana ya miziki, mahojiano, maigizo ya sauti na vingine vingi ilimradi tu viwe katika mfumo wa sauti.

Platform hizi pia unaweza kuwa nazo mtu binafsi au kikundi au hata makundi zaidi ya moja kuweza kumiliki page au akaunti moja ambayo unaweza kuweka kazi zako na watu wengine katika mfumo wa sauti na kuanza kufata utaratibu wa kupata pesa kupitia kazi hizo.

UNAHITAJI YAFUATAYO ILI UWEZE KUTENGENEZA PESA KATIKA PLATFORM HIZI:
Hapa unahitaji vifaa kadhaa kulingana na aina ya audio/ sauti unazotaka kupakia (upload) kwenye hizi platform lakini kwa wanaotaka kupakia miziki tu au sauti ambazo tayari zipo katika mfumo wa audio basi unapaswa kuwa na vifaa vifuatavyo: computer, simu aina ya smart phone, zaidi sana unahitaji kuwa na internet aidha iwe ya kuunga kwa bando za simu au rooter vyovyote vile.

Licha ya kuwa na hivyo vyote bado inahitaji pia jambo lingine litakalo kupa uwezo mkubwa wa kupata pesa kutoka huku nalo ni uwe mtu wa kupenda miziki au maswala ya Burudani na udaku kidogo au una tabia na malengo kama ya wale youtubers maana mambo haya ndio yanauzika sana katika soko la platform hizi vinginevyo unaweza kuona mambo magumu kwa sababu nje na hapo soko litakupita nje.

KAZI NA PESA ZINAANZIA HAPA 
Baada ya kuwa na haya yote kinachofata ni kufungua akaunti katika moja ya platform hizi aidha soundcloud au audio mack, kisha utachagua aina ya audio unazotaka kupakia (upload) huko unaweza kuchanganya au kuweka miziki na nyimbo tu, ni wewe tu unavyaamua. Kuapload hizo audio na kuzipa caption au majina utakavyo na mwisho kabisa ili upate hela tunairuhusu akaunti yako iweze kukupa nafasiya wewe kulipwa kutokana na hizo kazi zako kwa maana ya kuimonetize.

Endelea kubaki na gericmedia.com ili tuzifanye hatua tajwa hapo juu kwa pamoja katika machapisho yajayo. Jisajili kwa kuweka email yako ili uweze kupata kila chapisho linapowekwa hapa. Kwa maswali, ushauri au maoni wasiliana nasi kwa simu/text/whatsApp: 0743536577 au barua pepe: gericml@gmail.com 



PESA ZIKO HAPA (SOUND CLOUD) (Part 2) PESA ZIKO HAPA (SOUND CLOUD)  (Part 2) Reviewed by DjGeric on October 24, 2018 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.